Add parallel Print Page Options

Yesu Afundisha na Kuponya Watu

(Lk 6:17-19)

23 Yesu alikwenda sehemu zote za Galilaya, akifundisha na akihubiri Habari Njema katika masinagogi kuhusu Ufalme wa Mungu. Aliponya magonjwa yote na madhaifu mengi ya watu. 24 Habari kuhusu Yesu zilienea katika nchi yote ya Shamu, na watu waliwaleta wale wote wenye kuteswa na magonjwa na maumivu mbalimbali. Baadhi yao walikuwa na mashetani, wengine walikuwa na kifafa na wengine walikuwa wamepooza. Yesu akawaponya wote. 25 Makundi makubwa ya watu walimfuata; watu kutoka Galilaya, na jimbo lililoitwa Miji Kumi,[a] Yerusalemu, Yuda na maeneo ng'ambo ya Mto Yordani.

Read full chapter

Footnotes

  1. 4:25 Miji Kumi Jimbo hili lilikuwa mashariki ya Ziwa la Galilaya na wakazi wake hawakuwa Wayahudi. Miji Kumi imejulikana pia kama Dekapoli.