Add parallel Print Page Options

Pilato Ajaribu Kumwachia Huru Yesu

(Mk 15:6-15; Lk 23:13-25; Yh 18:39-19:16)

15 Kila mwaka wakati wa Pasaka, gavana angemwachia huru mfungwa mmoja yeyote ambaye watu wangetaka aachiwe huru. 16 Wakati huo alikuwepo mtu gerezani aliyejulikana kuwa ni mtu mbaya. Mtu huyu aliitwa Baraba.

17 Kundi la watu lilipokusanyika, Pilato aliwaambia, “Nitamwacha huru mtu mmoja. Mnataka nani nimwache huru: Baraba au Yesu aitwaye Masihi?” 18 Pilato alijua kuwa viongozi wa makuhani na viongozi wazee wa Kiyahudi walimkabidhi Yesu kwake kwa sababu walikuwa wanamwonea wivu.

19 Pilato alipokuwa ameketi kwenye kiti cha hukumu, mkewe akamtumia ujumbe uliosema, “Usifanye jambo lolote juu ya huyo mtu. Hana hatia. Nimeota ndoto juu yake usiku, na ndoto hiyo imenihangaisha sana.”

20 Lakini viongozi wa makuhani na viongozi wazee wa Kiyahudi waliwaambia watu waombe Baraba aachiwe huru na Yesu auawe.

21 Pilato akasema, “Nina Baraba na Yesu. Je, mnataka nimwache huru yupi?”

Watu wakajibu, “Baraba!”

22 Pilato akauliza, “Sasa nimfanye nini Yesu, aitwaye Masihi?”

Watu wote wakasema, “Mwue msalabani!”

23 Pilato akauliza, “Kwa nini mnataka nimwue Yesu? Amefanya kosa gani?”

Lakini walipaza sauti wakisema, “Mwue msalabani!”

24 Pilato akaona hakuna jambo ambalo angefanya ili kubadili nia yao. Kiukweli ilionekana wazi kuwa kungetokea fujo. Hivyo alichukua maji na kunawa mikono yake[a] mbele yao wote. Akasema, “Sina hatia na kifo cha mtu huyu. Ninyi ndio mnaofanya hili!”

25 Watu wakajibu, “Tutawajibika kwa kifo chake sisi wenyewe na hata watoto wetu!”

26 Kisha Pilato akamwachia huru Baraba. Na akawaambia baadhi ya askari wamchape Yesu viboko. Kisha akamkabidhi Yesu kwa askari ili akauawe msalabani.

Read full chapter

Footnotes

  1. 27:24 kunawa mikono yake Pilato alifanya hivi kama ishara kuwa hakuwa amekubaliana na hakushiriki jambo ambalo watu waliamua kufanya.