Add parallel Print Page Options

Yesu Asafisha Eneo la Hekalu

(Mk 11:15-19; Lk 19:45-48; Yh 2:13-22)

12 Yesu alipoingia katika eneo la Hekalu, aliwatoa nje wote waliokuwa wanauza na kununua vitu humo. Alizipindua meza za watu waliokuwa wanabadilishana pesa. Na alipindua viti vya watu waliokuwa wanauza njiwa. 13 Yesu aliwaambia, “Maandiko yanasema, ‘Hekalu langu litaitwa nyumba ya sala.’(A) Lakini mmelibadilisha na kuwa ‘maficho ya wezi’.(B)

14 Baadhi ya watu waliokuwa wasiyeona na walemavu wa miguu walimjia Yesu alipokuwa eneo la Hekalu, naye aliwaponya. 15 Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria waliona mambo ya ajabu aliyokuwa anatenda. Na waliona watoto walivyokuwa wanamsifu wakisema, “Sifa kwa Mwana wa Daudi.” Mambo haya yote yaliwakasirisha makuhani na walimu wa sheria.

16 Wakamwuliza Yesu, “Unasikia wanayosema watoto hawa?”

Akajibu, “Ndiyo. Maandiko yanasema,

‘Umewafundisha watoto wadogo na watoto
    wanyonyao kusifu.’(C)

Hamjasoma Maandiko haya?”

17 Kisha Yesu akawaacha na akaenda katika mji wa Bethania akalala huko.

Read full chapter