Add parallel Print Page Options

Zingatieni Nuru

(Lk 8:16-18)

21 Yesu akawaambia, “Unapoileta taa ndani[a] je unaiweka chini ya bakuli ama uvungu wa kitanda? Au unaileta ndani na kuiweka juu ya kitako cha taa? 22 Kwani kila kilichofichika kitafunuliwa, na kila kilicho cha siri kitatokea kweupe kwenye mwanga. 23 Yeyote mwenye masikio mazuri ni bora asikie.” 24 Kisha akawaambia, “Zingatieni kwa makini kile mnachokisikia. Kwani jinsi mnavyosikiliza kwa makini, ndivyo mtakavyoelewa na kuzidi kuelewa. 25 Kwa kuwa kila aliye na uelewa kidogo ataongezewa zaidi. Lakini wale wasiosikiliza kwa makini watapoteza hata ule uelewa mdogo walio nao.”[b]

Read full chapter

Footnotes

  1. 4:21 taa ndani Yesu anafananisha mafundisho yake kama taa iliyoletwa chumbani penye giza.
  2. 4:25 Kwa kuwa … nao “Mtu anapoleta taa chumbani, haiweki chini ya kikapu au chini uvunguni mwa kitanda! Badala yake, anaiweka mahali pa juu chumbani. 24 Mzingatie kwa makini kile mnachokisikia. Jinsi mnavyosikiliza kwa makini, ndivyo mtakavyoelewa. Na Mungu atawawezesha muelewe zaidi. 25 Watu walio na uelewa kidogo watapokea zaidi, lakini wale ambao hawakusikiliza vizuri, hata ule uelewa mdogo waliyonao nao utaondolewa kwao. Watasahau kidogo walichoelewa.”