Add parallel Print Page Options

15 Yesu akawaambia, “Nilitaka sana kula mlo huu wa Pasaka pamoja nanyi kabla sijafa. 16 Sitakula mlo mwingine wa Pasaka mpaka itakapopewa maana yake kamili katika ufalme wa Mungu.”

17 Kisha Yesu akachukua kikombe kilichokuwa na divai. Akamshukuru Mungu, na akasema, “Chukueni kikombe hiki na kila mmoja anywe. 18 Sitakunywa divai tena mpaka Ufalme wa Mungu utakapokuja.”

19 Kisha akaichukua baadhi ya mkate na akamshukuru Mungu. Akaigawa vipande vipande, akawapa vipande mitume na kusema, “Mkate huu ni mwili wangu ninaoutoa kwa ajili yenu. Kuleni kwa kunikumbuka.” 20 Katika namna ile ile, baada ya kula chakula, Yesu akachukua kikombe chenye divai na akasema, “Divai hii inawakilisha Agano Jipya kutoka kwa Mungu kwa watu wake. Litaanza pale damu yangu itakapomwagika kwa ajili yenu.”[a]

Read full chapter

Footnotes

  1. 22:20 Nakala chache za Kiyunani hazina maneno ya Yesu katika sehemu ya mwisho ya mstari wa 19 na mstari wote wa 20.