Add parallel Print Page Options

Yesu Anaingia Yerusalemu Kama Mfalme

(Mt 21:1-11; Mk 11:1-11; Lk 19:28-40)

12 Siku iliyofuata watu waliokuwamo Yerusalemu walisikia kwamba Yesu alikuwa anakuja huko. Hili ni kundi la watu waliokuja kusherehekea sikukuu ya Pasaka. 13 Hawa walibeba matawi ya miti ya mitende na kwenda kumlaki Yesu. Pia walipiga kelele wakisema,

“‘Msifuni[a] Yeye!’
‘Karibu! Mungu ambariki yeye
    ajaye kwa jina la Bwana!’(A)
Mungu ambariki Mfalme wa Israeli!”

14 Yesu akamkuta punda njiani naye akampanda, kama vile Maandiko yanavyosema,

15 “Msiogope, enyi watu wa Sayuni![b]
Tazameni! Mfalme wenu anakuja.
    Naye amepanda mwana punda.”(B)

16 Wafuasi wa Yesu hawakuyaelewa yale yaliyokuwa yanatokea wakati huo. Lakini Yesu alipoinuliwa juu kwenye utukufu, ndipo walipoelewa kuwa haya yalitokea kama ilivyoandikwa juu yake. Kisha wakakumbuka kwamba walifanya mambo haya kwa ajili ya Yesu.

17 Siku Yesu alipomfufua Lazaro kutoka wafu na kumwambia atoke kaburini walikuwepo watu wengi pamoja naye. Hawa walikuwa wakiwaeleza wengine yale aliyoyafanya Yesu. 18 Ndiyo sababu watu wengi walienda ili kumlaki Yesu; kwa kuwa walikuwa wamesikia habari za ishara hii aliyoifanya. 19 Mafarisayo nao wakasemezana wao kwa wao, “Tazameni! Mpango wetu haufanyi kazi. Watu wote wanamfuata Yesu!”

Read full chapter

Footnotes

  1. 12:13 Msifuni Kwa maana ya kawaida, “Hosanna”, ambalo ni neno la Kiebrania lililotumika kumwomba msaada Mungu. Hapa, labda ilikuwa ni kelele ya shangwe iliyotumika kumsifu Mungu au Masihi wake.
  2. 12:15 watu wa Sayuni Kwa maana ya kawaida, “binti Sayuni”, ina maana mji wa Yerusalemu. Tazama Sayuni kwenye Orodha ya Maneno.